Kati ya vijana wanaoiishi Itikadi ya UTU ambayo misingi yake ni Udugu, Maadili, Usawa, Haki, Imani, Mabadiliko, Uhuru,Wajibu, Asili, Kazi na endelezo ndani ya Mkoa wa Kigoma huwezi kuacha Kumtaja Wiston Andrew Mogha Mwanamageuzi aliye tayari kukifia chama chake.

Je, Wiston Andrew Mogha ni nani?

Wiston Andre Mogha ni muasisi wa chama cha ACT –Wazalendo mwenye kadi namba 28. Mnamo mwaka 2014 akiwa chama cha ACT Wazalendo alikuwa ni miongozi mwa vijana wachache Kati ya 12 walioenda kwa msajili kusajili chama na kupatiwa usajili wa kudumu.

Wakati huo Ikumbukwe Wiston Mogha ni Mwanachama wa kwanza wa ACT-wazalendo aliyewekwa ndani kwa sababu ya shughuli za chama wakati wa kueneza chama hicho.

Wiston Mogha akiwa chama cha ACT Wazalendo aliwahi kugombea ujumbe wa kamati kuu na kushindwa kwa madai ya kuwa yeye ni kijana mdogo. Hivyo walihitaji kupunguza idadi ya watu wa kigoma kwenye ngazi za maamuzi ya chama kutokana na kiongozi wa chama alikuwa mtu wa kigoma, Makamu Mwenyekiti alikuwa mtu wa kigoma, mjumbe wa kamati kuu wa kuteuliwa alikuwa mtu wa kigoma.

Safari ya Wiston Mogha iliendelea na hakukata tamaa aliendelea kukitumikia chama. Sekretarieti ilipendekeza awe mwenyekiti wa ngome ya vijana taifa kupitia ACT-Wazalendo na kuonesha kuifurahia nafasi  hiyo kabla ya kuletewa taarifa kutoka kwa wajumbe wa sekretarieti kuwa yeye ni mtu wa kigoma na wanahitaji kupunguza watu wa kigoma hivyo nafasi anayo hihitaji apewe mtu mwingine.

Septemba 24, 2014, Wiston Mogha ambaye pia ni mmiliki wa hostel ya Awimo iliyopo Kigoma mjini, alitangaza kugombea Ubunge kwenye jimbo la kigoma mjini. Sekretarieti ya chama chake cha ACT walishindwa kumpa haki hiyo kwa kisingizio kuwa ni mapema mno kutangaza nia hiyo kwa kuwa alikuwa kijana mdogo huku sababu nyingine ikitajwa kuwa Kiongozi mkuu wa Chama hicho Ndugu Zitto Kabwe (Mb) alikuwa akiliwania Jimbo la kigoma Mjini kwa ud na uvumba.

Akiwa Mkoani Shinyanga, Ndugu Zitto Kabwe (Mb), Habibu Mchange na Msafiri Mtemelwa walimuomba asigombee kigoma na agombee Jimbo la kawe jijini Dar es salaam kwakuwa kuna watu wengi wa kigoma wanaishi humo na kumuachia Ndugu Zitto Kabwe agombee Kigoma Mjini, hali iliyompelekea ndugu Mogha kuachana na jimbo hilo na kumuahidi kumpigania kiongozi wake mkuu Ndugu Zitto Kabwe katika kampeni zake za kuwania ubunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi wa 2015.

Kaimu Mwenyekiti NCCR-Mageuzi Kigoma Mjini Ndg. Wiston Mogha.

Wiston Mogha na kofia ya Uenyekiti ndani ya NCCR-Mageuzi Kigoma.

Hivi sasa Wiston Mogha ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Jimbo la Kigoma Mjini.

Mwenyewe anasema, kilichomuondoa ACT-Wazalendo ni siasa za wivu na chuki dhidi yake. Na kukiri kuwa changamoto hizo zimempa nguvu ya kuendeleza mapambano ya haki na uhuru ili kuifanya jamii iweze kuishi kwenye misingi ya UTU.

Akiwa kama kaimu mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Kigoma, Wiston Mogha kwa kipindi cha miezi 2 tu amejizolea wafuasi wengi kutoka vyama mbalimbali huku idadi yake ikitajwa kufikia wafuasi 428 na hivyo kuwa na jumla ya wanachama zaidi ya 29,923 wa NCCR-Mageuzi Kigoma Mjini.

Mwenyewe amenukulia akisema, siasa za mkoa wa Kigoma wanaamini katika siasa za kimageuzi alisema Mwenyekiti huyo wa chama Jinbo la kigoma Mjini Wiston Mogha.

 “Tunayo nafasi ya kufanya mabadiliko hakuna haja ya kufanya siasa za vurugu hasa siasa za kimageuzi za kujitoa pamoja na utulivu” Alisema Wiston Mogha

Hata hivyo Makamu Mwenyekiti huyu wa Jimbo la kigoma Mjini Ndugu Wiston Mogha anaendelea kuamini kuwa ipo siku atagombea ubunge na kutimiza dhamira yake ya kuwatumikia wananchi.