Vuguguvu la mageuzi limeendelea kushika kasi ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi nchini huku watanzania walio wengi wakiwa na matumaini ya kufika sayuni.

April 25, 2020, chama chetu (NCCR-Mageuzi) kimepokea wanachama wapya zaidi ya 83 kutoka vyama vya upinzani kwenye kata ya Buzebazeba Mjini Kigoma.

Ni ukweli usiopingika kigoma ni ngome ya NCCR-Mageuzi na ni baba wa mageuzi  nchini kutokana na kuimarika kwa chama chetu na kurudi kuwa na mvuto na kupokea watanzania wengi na wenye kuamini katika sera ya Itikadi ya Utu.

Zoezi la utoaji wa kadi za Uanachama kwa wanachama wapya wanaojiunga na NCCR-Mageuzi

Hata hivyo chama chetu katika misingi ya kikatiba inaamini kuwa njia bora ya kuleta mageuzi na kuongoza serikali katika kuleta mabadiliko chaya katika jamii yetu kwa amani, hiari na nguvu ya hoja itokanayo na itikadi ya sera zetu zinazolenga kuwakomboa wanyonge na kuwaongeza wapate maendeleo na ustawi wa taifa letu.

Ikumbukwe kuwa utulivu uliopo ndani ya chama chetu hivi sasa kwa kusimamia Itikadi ya UTU ndiyo unaowarejesha wapinzania nchini.

Zoezi la kupokea wanachama wapya limefanyika na katibu wa jimbo la kigoma Mjini (NCCR-Mageuzi) Ndugu. Frank Ruhasha pamoja na kaimu mwenyekiti Jimbo la kigoma mjini Wiston Mogha, huku wanachama wapya wakionesha Imani kubwa kwa chama chetu.

Hivi sasa jimbo la kigoma limeendelea kujizolea wafuasi wengi kutoka vyama vingine vya upinzani kujiunga na chama chetu cha NCCR-Mageuzi na kufikia idadi kubwa ya wanachama wapya kwa kipindi cha muda mfupi.

Mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi akisubiri kukabidhiwa kadi yake ya Uanachama