Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo Ndugu JAMES FRANCIS MBATIA amezitaka mamlaka zinazosimamia uchaguzi kuwatendea haki Watanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba ili kupata viongozi wanaostahili kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.

Ndugu Mbatia ameyasema hayo katika mkutano maalumu na wanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi Mkoa wa Arusha, uliofanyika Juni 10, 2020 Jijini Arusha na kushuhudia chama kikiwapokea wanachama wapya zaidi ya 32,102.

Katika mkutano huo Ndugu Mbatia amezitaka mamlaka za uchaguzi kusimamia uchaguzi kwa uhuru na haki huku watanzania wakitakiwa kuchagua viongozi wanaostahili, wenye uwezo, wacha Mungu na wanaochukia maovu katika jamii kwa maslahi ya Watanzania wote.

Katika hatua nyingine Viongozi wa dini wametakiwa kutoa mafundisho yatakayowasaidia watanzania kupata viongozi watakao wavusha na kulitumikia taifa hili kwa uadilifu.

Sanjali na hayo Ndugu Mbatia amewataka watanzania kutambua kuwa Upinzani katika siasa sio uadui, hoja za maendeleo zinatatuliwa kapitia meza ya maridhiano ili watanzania wapate kunafaika na uongozi bora.

Itakumbukwa kuwa mpaka sasa chama kinachowaunganisha watanzania na Utu wao ni chama cha NCCR Mageuzi katika haki msingi ya kuwaleta watanzania wote kwa pamoja kwa kuzingatia misingi ya maadili pamoja na uzalendo.