Katika kutimiza sheria ya vyama vingi nchini Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania{ORPP}imetembelea ofisi ya chama cha NCCR MAGEUZI makao makuu kwa ajili ya kufanya uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kwa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Zoezi hilo limetekelezwa na Naibu Msajili wa vyama vya siasa nchini Ndg,Sisty Nyahoza , Mkaguzi wa ndani kutoka Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Ndg. Emanuel Maina pamoja na afisa habari Ndg.Abuu Kimaro ikiwa ni utekelezaji wa kudumu wa majukumu ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria za gharama za uchaguzi.

Mkaguzi wa ndani kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Ndg. Emanuel Maina akisikiliza wasilisho la rejesta ya wanachama wa NCCR-Mageuzi

Moja ya mambo yaliyofanyika kwenye ofisi za NCCR MAGEUZI makao makuu ni pamoja na Uhakiki wa:

 1. Ofisi ya makao makuu.
 2. Uwepo wa anuani ya chama inayotumika.
 3. Uwepo wa barua pepe ya chama.
 4. Uwepo wa cheti cha usajili wa chama na cheti cha usajili wa bodi ya wadhamini wa chama.
 5. Uwepo wa katiba,kanuni,nembo ya chama na bendera ya chama katika ofisi husika.
 6. Uhai wa uongozi wa kitaifa wa chama.
 1. Idadi ya wanachama.
 2. Uwepo wa mtunza fedha za chama.
 3. Uwepo wa orodha yawaajiriwa wa chama.
 4. Taarifa za mwisho wa mwaka wa fedha.
 5. Uhai wa kisheria wa bodi ya wadhamini ya chama
 6. Uwepo wa rejesta za chama zinazohitajika na sheria ya vyama vya siasa ikionesha jina kamili la mwanachama, namba ya kadi ya uanachama, umri,jinsi, anuani ya makazi,wilaya na mkoa anaoishi.

Afisa habari ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Ndg.Abuu kimaro

Hata hivyo ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kupitia miongozo ya chama hususani katika kuelekea uchaguzi mkuu 2020 hufanya uhakiki wa vyama ili  Kufuatilia utendaji wa vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992.Kwa kuwa kiungo kati ya Serikali na Vyama vya Siasa nchini.

Mara baada ya mapitio hayo Naibu msajili wa vyama vya siasa nchini ndg.Sisty Nyahoza amekishauri chama kuendelea kutii maagizo yanayotolewa na Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kusema hana mashaka na chama cha NCCR-MAGEUZI kulingana na kuiishi itikadi ya uti kwa kutanguliza maslahi ya watanzania wote.

picha ya pamoja ya viongozi wa chama cha NCCR-MAGEUZI na viongozi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.