Hivi karibuni kumekuwa na minyukano ya nani bora kuliko mwengine katika ulingo wa siasa za upinzani ndani ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli.

Tumeshuhudia baadhi ya mijadala ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini wakijinasibu namna watakavyowavusha watanzania dhidi ya serikali ya awamu ya tano.

Wimbi kubwa la hamahama ya viongozi pamoja na wanachama kutoka chama kimoja kwenda kingine na kutoa madhaifu ya vyama walivyokuwa wanaviongoza limekuwa kubwa huku hoja kubwa ikiwa ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya vyama hivyo.

Ni jambo la kawaida sana kushuhudiwa kila tunapokaribia uchaguzi mkuu, ambapo Oktaba 2020 mwaka huu ni siku ambayo watanzania watachagua waakilishi wa kuwaongoza kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge pamoja na Urais.

Hivi karibuni Chama cha NCCR Mageuzi kimejizolea umaarufu mkubwa wa kupokea wanachama wengi wanaoomba ridhaa ya kujiunga na chama hicho kwa kuwa ndio chama kinachosimamia misingi ya Itikadi ya UTU wa binadamu.

Swali la kujiuliza, tufani hiyo inayotarajiwa kutokea haiwezi kuwa kama ile ya uchaguzi waserikali za mitaa..? Itakumbukwa kuwa kutoshiriki kwa upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana kumeshindwa  kutoa taswira ya namna gani viongozi wa upinzani wanakubalika na wananchi na hivyo 2020 ni ngumu kutabiri ushawishi wao katika kuchukua dola japo kwa asilimia kubwa chama cha NCCR Mageuzi kimeonekana kuwavutia mamia ya walio wengi kulingana na sera zake.

Ni ukweli usiopingika Upinzani wa Chadema na ACT wazalendo dhidi ya Chama cha NCCR Mageuzi umeendelea kuibomoa Chadema na ACT kwa kukosekana demokrasia wakati wao ndio wahubiri wa demokrasia kwa kuikosoa serikali ya CCM bila kutazama mzizi unaowatafuna wao wenyewe ndani kwa viongozi wao kuhama kutoka vyama vyao na kuhamia NCCR Mageuzi.

Ni ukweli usiopingika chama huzaliwa na kufa na kuzaliwa tena ndivyo ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi kwa kuiishi itikadi ya Utu.

katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Udiwani,Ubunge na Urais Mwaka huu chama cha NCCR-Mageuzi kimeendelea kujiimarisha kiuongozi pamoja na sera zitakazo wavusha watazania kutoka hapa walipo na kufika nchi ya Ahadi.