“NCCR-Mageuzi tuna mikakati mizuri sana ya kuhakikisha Kanda ya Ziwa inakuwa sehemu ama ngome ya NCCR-Mageuzi. Awali kabla ya CHADEMA na vyama vingine kuja vizuri NCCR-Mageuzi ngome yake ilikuwa kanda ya ziwa. Maelfu ya wanachama wanaohama sasa hivi kwenye vyama mbalimbali vya siasa na kuja NCCR-Mageuzi wanarudi kwenye asili yao, Siasa ni kama maji hauwezi kuyazuia kwenye njia yake”-Ndugu Edward Julius Simbeye.

Ni maneno machache mno yenye kufikirisha na kupasua vichwa vya watu mbalimbali. Ndio, unajua ninachomaanisha. Ni Ukweli wa wazi kuwa Siasa ni kama maji tu yanahitaji kupita kwenye njia yake na utakapojaribu kuziba njia ni wazi unatengeneza mafuriko yasiyozuilika kwenye makazi ya watu na utakuwa kero miongoni mwao.

Hii ni sawa na kilichotokea huko Mkoani Mara. Ni wazi sasa wananchi wameelewa na kufahamu vyema Itikadi ya UTU, wimbo unaoimbwa na Chama chenye kujali haki, maadili na Usawa, si kingine ni NCCR-Mageuzi. Na sasa wananchi wanahitaji kurudi kwenye asili yao, nani anataka kuzuia maji yasipite kwenye njia yake?

Ndani ya masaa 48 pekee tayari chama cha NCCR-Mageuzi kilitangaza kupokea zaidi ya wanachama 24,680 kutoka Chadema pamoja na viongozi wa juu zaidi ya 19 wote kutoka Wilaya ya Bunda akiwemo aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara Ndugu Daniel Ayote, aliyekuwa Afisa wa Oganaizesheni Kanda ya Serengeti Ndugu Frank Kubwera, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Bunda Ibrahim Kibwe na wengine kibao.

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma NCCR-Mageuzi Taifa Ndugu Edward Simbeye Kulia akimkabidhi kadi ya Uanachama aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mara ndugu Daniel Ayote

Hii ilikuwa habari ya kuhuzunisha sana hasa kwa wale ambao hawapendi maji yapite kwenye njia yake. Masaa machache taarifa zilienea kuwa;

Gari la Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma NCCR-Mageuzi Taifa Ndugu Edward Julius Simbeye limevamiwa na kupigwa mawe na wanaosadikika kuwa ni kundi la Wafuasi wa Chadema alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kichama Wilayani Tarime, Mkoani Mara.

Ni wazi sasa hofu na mashaka imetanda kwa watu wasiopenda kuona maji yanapita kwenye njia yake. Hii inaamsha hali mpya sasa kwa wananchi dhidi ya muovu yule anayetaka kuleta mafuriko kwenye makazi ya watu.

Masaa machache mara baada ya Kuvamiwa kwa gari la kiongozi wa NCCR-Mageuzi, wananchi wanashindwa kujizuia, Wilayani Tarime wanachama wa CHADEMA wamechukizwa na fujo zilizofanywa na wafuasi wa chama chao na kuamua sasa kwa wingi kujiunga na NCCR-Mageuzi

Tukio hilo limetokea masaa machache tu baada ya viongozi wenye ushawishi mkubwa na waasisi wa Chadema Tarime, ndugu Eliasi Nyagabona, aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Uchaguzi, Sera, Ilani na Utafiti Chadema Kanda ya Serengeti pamoja na aliyekuwa Diwani Viti Maalumu Chadema Bi. Marry Nyagabona kutaganza kung’atuka na kuachia nyadhifa zao zote ndani ya Chadema na kujiunga na NCCR-Mageuzi. Na baadaye,

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CHADEMA Wilaya ya Butiama na kuwa Mwenyekiti wa Kata ya Nyakanga ndugu Philimoni Wesaka akajiunga rasmi na NCCR-Mageuzi kwa kile alichokisema kuwa ni kutofurahishwa na vurugu zilizofanywa na Chama chake cha CHADEMA Wilayani Tarime.

Mkuu wa idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma Taifa Ndugu Edward Simbeye kushoto akimkabidhi kadi ya Uanachama aliyekuwa M/kiti wa Wazee wa CHADEMA Wilaya ya Butiama na Mwenyekiti wa Kata ya Nyakanga ndugu Philimoni Wesaka

Wakati huo huo aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na Muweka hazina wa Kata ya Nyakanga Wilaya ya Butiama Kupitia CHADEMA ndugu Ubwere Kitare naye akajivua nafasi zake zote za Uongozi na kuamua kujiunga na NCCR-Mageuzi.

Sambamba na viongozi hao, Mwanachama mwandamizi wa CHADEMA Wilaya ya Butiama ndugu Kamuru Paul nae amejiunga na NCCR-Mageuzi na kukabidhiwa Kadi na Mkuu wa idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma Ndugu Edward Simbeye.

Ni wazi sasa wananchi wanachoshwa na siasa za fujo, ugomvi na vurugu. Na ni wazi sasa wananchi wameamua kurudi kwenye asili yao, na kuacha maji yapite kwenye njia yake.

Je, ni nani mwenye kuweza kuzuia maji yasipite kwenye njia yake?

 

Alichokisema aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Uchaguzi, Sera, Ilani na Utafiti Chadema Kanda ya Serengeti ndugu Eliasi Nyagabona