Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais Oktoba, 2020, chama cha NCCR-Mageuzi kimeendelea kujiimarisha kiuongozi kwa kupata zaidi ya wanachama wapya elfu 60,000 kwa kipindi cha Muda mfupi

kumekuwepo na maneno mengi yanayozungumza huko duniani ya kuwa viongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi kutumika na chama cha CCM jambo ambalo siyo sahihi. Ukipitia katiba ya chama cha NCCR-MAGEUZI Sura ya pili ya MISINGI YA KISIASA Kipengele cha kwanza kinasema chama chetu “Kinakubali itikadi ya UTU ambayo lengo lake ni ujenzi wa jamii yenye Uhuru, Uzalendo, Uadilifu,Umoja, Uwazi, Uwajibikaji,Haki za binadamu,Usawa na ustawi wa jamii inayokubali kutegemeana kwa binadamu katika msingi wa mmoja kwa wote na wote kwa umoja pamoja na kifungu cha 6 kinachosema “Kupenda kushirikiana na watu, jamii na vyama vyenye kuamini na kutetea itikadi ya UTU au madhumuni yanayoshabihiana na yale ya chama chetu”.

Hivi karibuni  kumekuwa na hamasa kubwa ya viongozi kutoka chama cha CHADEMA, ACT pamoja na CCM kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi. Wiston Mogha ni mmoja wa wanachama kutoka ACT-Wazalendo na muasisi wa chama hicho mwaka 2014 mwenye kadi number 28 amejiunga na NCCR-Mageuzi.

Katika hotuba yake kwa vyombo vya habari Mogha amesema katiba ya ACT-Wazalendo kwa kiasi kikubwa imebadilishwa ili kuwanufaisha wachache ukitofautisha na katiba ya awali ambayo ilikuwa ikieleza ukomo wa uongozi lakini kwa sasa haina ukomo wa Uongozi.

Mwenyekiti NCCR-Mageuzi Kigoma Mjini Ndg. Wiston Mogha.

Wiston Mogha aligombea Uwenyekiti wa ngome ya vijana Taifa na kusema alishindwa kupata nafasi hiyo kutokana na maelekezo kutoka kwa viongozi kuwa hawamtaki kwa kuwa anatumiwa na chama tawala hatua iliyosababisha tarehe 18 march 2020 kujivua uanachama wa ACT Wazalendo na tarehe 03 Aprili 2020 kutangaza kujiunga na NCCR Mageuzi.

Kwa upande wake FRANK LUHASHA kutoka CHADEMA amesema amekuwa katika chama hicho kwa zaidi ya miaka 13 na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika mkoa wa kigoma na kuamua kukimbia chama chake kutokana na siasa zinazofanywa kukosa Itikadi ya UTU.

Hata hivyo Ruhasha amesema kwa sasa NCCR ndicho chama pekee chenye siasa mbadala kinachotumia upole kuwaunganisha watanzania kwa misingi ya itikadi ya UTU.

Kwa upande wake mratibu wa umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini {CHASO} Ndiholeye Zuberi Kifu aliondoka CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi March 22 na sababu za kutokuwa na usawa wa kijinsia katika nyadhifa za kiuongozi.

‘Tumeshuhudia watu wakiondolewa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi bila kuelezwa sababuza kufanya hivyo tumeshuhudia vitendo vya rushwa, upendeleo na uvunjwaji wa katiba ya chama ya mwaka 2006’- alisema Ndiholeye Zuberi Kifu’.

Antony Calist Komu ni Mbunge wa moshi vijijini kupitia Chadema naye ameomba ridhaa ya kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi kwakuwa ndicho chama pekee kinachosimamia itikadi ya UTU kwa maslahi mapana ya watanzania.

Hivi karibuni chama chetu kimepokea wanachama wapya kutoka mkoa wa Dodoma, Mtwara, Singida, Kigoma,shinyanga pamoja na Ruvuma wakiomba ridhaa ya kujiunga na chama chetu.

Swali la kujiuliza je.?Watanzania hawa wanaoendelea kujiunga na cha a chetu na kuitwa ni wasaliti, ni wasaliti kwa nani.? Je hao siyo raia waTanzania.? Na Je.Hawana haki ya kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi?

Ikumbukwe kuwa taarifa za uongo, uchochezi,uzandiki,Majungu na zenye kujenga chuki ndani ya jamii zinaletwa na kusambazwa na mahasimu  wetu wa kisaisa ambao hawana nia njema na chama chetu.