Wahenga walisema kuishi kwingi ni kuona mengi ndivyo inavyoishi katiba ya chama cha NCCR MAGEUZI tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992 pamoja na viongozi wake.

Mwenyekiti Taifa NCCR- MAGEUZI, Ndg James Mbatia yupo ziarani mkoani Mbeya kwa siku nne kukijenga chama. Kwenye ziara hiyo Mwenyekiti atapokea wanachama wapya, kuzindua ofisi ya kanda mkoa wa mbeya pamoja na kujua changamoto za wakazi wa mkoa wa Mbeya. Atatoa pia maelekezo pamoja na semina kwa wanachama na viongozi wa chama ili kuishi misingi ya NCCR MAGEUZI ya UTU NI NGAO YETU

Ziara hiyo liyoanza jana tarehe 04/03/2020 Mwenyekiti aliambatana na mjumbe wa halmashauri kuu Ndg Rajabu Kazimoto, kamishina wa chama wa mkoa wa Mbeya Ndg Bonifasi Mwabukusi pamoja na waandishi wa habari.

Baada ya kupokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Ndg Mwenyekiti alipata nafasi ya kuhojiwa na waandishi wa habari na kisha kuelekea studio za Baraka FM ambapo alizumgumza na wakazi wa jiji la Mbeya akielezea nia ya ziaza yake kabla ya kuelekea ofisi za mkuu wa Mkoa wa Mbeya kukamilisha taratibu za kiserekali kabla ya ziara.

Kwenye mazungumzo yake na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Mwenyekiti alisisitiza kuwepo kwa mshikamano, upendo na amani katika taifa. Alisema NCCR – Mageuzi kama chama kinaongozwa, kusimamia na kusishi itikadi ya UTU na kuhakikisha malengo ya nchi yetu (mama Tanzania) yanafikiwa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimpongeza Mwenyekiti na kusema amefanya Jambo la busara kutembelea ofisi yake kwa ajili ya taratibu za ziara huku akisema NCCR – Mageuzi ni chama pekee cha upinzani kinachoongozwa kwa maadili na kufuata taratibu pasipo kuvunja sheria za nchi.

Akiwa wilayani Rungwe, lilijitokeza kundi kubwa la watu wakiomba ridhaa ya kujiunga na chama cha NCCR – Mageuzi ambapo Mwenyekiti alitoa nafasi na kisha kuwapokea wanachama wapya wapatao 255 kati yao 15 wakiwemo viongozi wa chama cha CHADEMA.

Mwenyekiti alitumia wasaa huo kusisitiza umuhimu wa mawazo mbadala kwenye maendeleo ya wakazi wa Rungwe na taifa nzima kwa ujumla huku akisema “tugange yajayo, NCCR – Mageuzi itashinda kwa hoja”

Wakati hayo yanaendelea, itakumbukwa kuwa NCCR MAGEUZI bado inasisitiza upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi pamoja na katiba mpya.

Imetolewa tar 05/03/2020