Chama cha NCCR MAGEUZI kimeendelea na harakati zake za kisiasa huku kikisimamia misingi na itikadi yake ya Utu ni Ngao Yetu. Katika ziara hiyo, Mwenyekiti alifanya mikutano ya ndani na kufungua matawi na ofisi ya chama hicho.

Akiwa Busokelo alipokea wanachama wapya zaidi ya 200 kutoka jimbo la Busokelo kata ya Mpombo, Luteba, kandete na Isange. Idadi hii inafanya jumla ya wanachama wapya waliopokelewa Mbeya kuwa zaidi ya mia tano tangu ziara ya Mwenyekiti ianze Mkoani Mbeya

Miongoni mwa wanachama waliojiunga na chama hicho na kukabidhiwa ni pamoja na viongozi wa zamani wa CHADEMA. Mingoni mwao ni Ndg Furaha Mwakalungwa na Ndg. Anyabwile Mwansile ambao walikuwa Mwenyekiti na katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye Jimbo la Busokelo.

Viongozi wengine wa CHADEMA waliohamia NCCR MAGEUZI ni pamoja na Ndg Edson Mwakilili ambaye alikuwa katibu mwenezi kata ya Mpombo, Ndg Asifiwe Mwatimba aliyekuwa katibu Mwenezi kata ya Kandete, Ndg Atupele Ngiluke katibu baraza la wazee kata ya Kandete. Wengine ni Ndg Gwantwa Mkumbi aliyekuwa katibu mwenezi kijiji cha Usanji, Ndg Nasibu Mwamaluka aliyekuwa mwenyekiti baraza la wazee kata ya Mpombo, Ndg Abokile Mwalema aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha chadema kijiji cha Kasanga, Ndg Samson Mwaitege aliyekuwa mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Kandete, Ndg John Mwandaga aliyekuwa katibu mwenezi chadema kata ya kandete pamoja na Ndg Nisile Mwaikenda aliyekuwa mjumbe BAWACHA.

Mara baada ya mwenyekiti kukabidhiwa kadi wanachama wapya, aliunda safu mpya ya viongozi wa muda mfupi ili kuendeleza shughuli za chama mahali hapo. Ndg Furaha Mwakalungwa aliteuliwa kuwa mwenyekiti jimbo huku Ndg Anyabwile Mwansile akiteuliwa kuwa katibu, wengine ni Ndg Uswege Mwamboma mkuu wa oganaizesheni na utawala, Ndg Tumaini Mwaikenda – Idara ya wanawake, Ndg Chirenga Mwambungu – Idara ya wazee pamoja na Ndg Kipesile Mwaikenda – Idara ya vijana.

Mwenyekiti aliutaka uongozi mpya kuheshimiana, kuamini na kulinda itikadi ya chama ya Utu huku wakitakiwa kuhubiri amani, mshikamano na maridhiano ya kisiasa yenye lengo la kuwapatia wana Busokelo maendeleo na kuacha kufanya majibizano na vyama vingine vya siasa.

Imetolewa tar 06/3/2020