Tangu kuasisiwa kwa vya vingi vya siasa mnamo mwaka 1992 chama cha NCCR -Mageuzi kimeendelea kusimamia itikadi ya utu. Itikadi ambayo lengo lake ni ujenzi wa jamii yenye uhuru,uzalendo,uadilifu,umoja,uwazi,uwajibikaji,haki za binadamu,usawa na ustawi wa jamii ya watanzania.

Itikadi ya utu ina misingi ya Kukubali na kuheshimu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Hii ni hatua iliyofikiwa katika mapambano ya kuleta demokrasia ya kijamii nchini.

mchango wa vyama na vikundi vingine vya kijamii katika kukuza na kudumisha demokrasia ya kweli ni  kuheshimu usawa wa haki ya kila mtu kisiasa,kiuchumi,kisheria na kijamii kwa kutambua haki za wanyonge ili waweze kujiendeleza kwa kasi zaidi

Itikadi ya utu inatutaka kuheshimu kazi na shughuli halali za watu binasfi katika Nyanja zote za kijamii na uchumi. Hii ni pamoja na kushirikiana na watu kupitia vyama vyenye kuamini na kutetea itikadi na maudhui yanayoshabihiana na chama chetu.