Karibu Watanzania NCCR-Mageuzi chama kinachojali UTU wa binadamu na viumbe hai wote hapa Duniani. Chama kinachoamini katika Diplomasia ya Maridhiano Amani na Utulivu wa Nchi yetu. Chama chetu kinalenga kuwa na Vijana wafuasi wa Amani na Umoja wetu kama Taifa, siasa za masuala baadala ya zile za kujadili watu na kujadili matukio. NCCR-MAGEUZI imejipanga kuwa na Taifa lenye Vijana wajuzi wa mambo, wabunifu na wenye weledi katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.  VIJANA wa NCCR-MAGEUZI endeleeni kuonesha siasa safi bila kusahau kuwa waadilifu katika maeneo yenu yote. Uadilifu ni sehemu ya Itikadi ya UTU.

Tarehe 11 na 12 Juni, 1991 vikundi mbali mbali vya watanzania waliokuwa wamedhamiria kuleta Mageuzi vilitisha kongamano jijini Dar es Salaam kudai mabadiliko katika mfumo wa siasa na serikali. Waliazimia kuunda kamati ya kitaifa kwa ajili ya mageuzi ya Katiba (National Committee for Constitution Reform), kwa kifupi NCCR. Kamati hiyo iliwahamasisha wananchi nchini kote juu ya hoja ya mageuzi ya kikatiba, na kuueleza mjadala wa umma na uchambuzi wa kisiasa hadi kuondolewa kwa mfumo wa chama kimoja na badala yake kuanzishwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vyingi.

Serikali ililazimika kuyakubali madai ya MAGEUZI na kupitisha marekebisho ya katiba ya kuruhusu siasa vya vyama vyingi nchini Tanzania. Marekebisho hayo yalifuta ibara iliyokuwa inatamka kuwa Tanzania ni nchi ya chama kimoja kwa kutungwa na kupitishwa kwa Sheria ya Vyama vya siasa, Na. 5 mwaka 1992. Hata hivyo, sheria hii ilihusu usajili na uendeshaji wa vyama vya siasa tu; sheria haikuvunja muundo tawala wa kimila wa mfumo wa chama kimoja. Kuanzia hapo vikundi kadhaa kutoka NCCR-Mageuzi viliunda vyama mbalimbali vya siasa vinavyojitegemea, na wanaharakati waliobaki ndani ya kamati waliazimia kuanzisha chama cha siasa kwa jina la NCCR – Mageuzi ( National Convention for Construction and Reform – Mageuzi) au kifupi NCCR ikabadilika na kuwa chama cha Mageuzi na Ujenzi wa Taifa ( National Convention for Construction and Reform – Mageuzi) au kwa kifupi NCCR – Mageuzi.

Tarehe 29 Julai, 1992 NCCR – Mageuzi kilipata usajili wa muda na tarehe 21 Januari, 1993 chama kikapata usajili wa kudumu kama chama cha siasa. NCCR – Mageuzi kinatambuliwa na mwasisi wa mageuzi ya kisiasa ya kidemokrasia na nchini Tanzania. Kwa hiyo matukio ya tarehe 15 Februari 1992 yalikuwa ni fursa ya kuimarika kwa vuguvugu la kidemokrsia katika karne ya Ishirini.

NCCR- Mageuzi ni chama cha aina mpya chenye dira na ujumbe; sifa ambayo inatakiwa kwa ajili ya changamoto ambazo zinalikabiliwa na changamoto ya kuvunja ngome ya mfumo wa kisiasa uliojengwa katika dhana ya muundo wa utawala wa chama kimoja. Mfumo huu unakwaza ukuaji wa demokrasia kwa vile hauruhusu mabadiliko yanayoweza kutoa fursa sawa kwa wadau wote katika mfumo mpya wa kisiasa nchini, na umeshindwa kufanya mabadiliko ya kikatiba ambayo ni muhimu katika ukuaji wa demokrasia. Changamoto hii ndio chachu ya NCCR – Mageuzi katika kuleta mabadiliko kwa kuchukua hatua zifuatazo:

 • Kukamata mamlaka ya dola kurejea uongozi bora
 • Kuwawezesha wazawa kuchukua, kudhibiti na kuendesha njia kuu za uchumi wa nchi
 • Kuongoza mapambano dhidi ya unyonyaji na dhuluma
 • Kuheshimu haki ya wananchi kuanzisha jumuiya zao, kuwa na ubunifu binafsi, na uhuru wa kujihusisha na mambo ya kijamii na kiuchumi
 • Kuhamasisha kufundisha na kutangaza itikadi ya UTU katika Nyanja ya siasa nchini Tanzania
 • Kuleta mabadiliko ya kimtazano katika nyanja za siasa, uchumi na jamii
 • Kushughulikia masuala ya maendeleo, mshikamano, umoja na amani ili kuboresha maisha ya Watanzania
 • Kuboresha agenda zake zianazohusu haki za binadamu (misingi ya demokrasia)
 • Kuboresha agenda zake kuhusu UTU
 • Dhamira ya kuendeleza mshikamano, amani na utengamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania na kujenga malengo kama haya ndani na nje ya Nchi.
 • Changamoto ya kuvunja ngome ya mfumo wa kiasa uliojengwa katika dhana ya muundo wa utawala wa chama kimoja ni sehemu tu ya malengo ya NCCR- MAGEUZI

 

Imeandaliwa na  WAJENZI WA TAIFA NCCR-MAGEUZI

 

#Itikadi yetu UTU

#UTU Itikadi yet

“PAMOJA TUTASHINDA “