Kuelekea Uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2020, ombwe la uchaguzi linazidi kushika kasi mara baada ya wabunge wengine wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Viti Maalum Bi. Joyce Bitta Sokombi na Bi. Susanne Peter Maselle kuomba ridhaa ya kujiunga na NCCR-Mageuzi mara baada ya Bunge kuvunjwa.

Hili ni pigo kubwa kwa chama hicho ikizingatiwa kuwa wabunge hao ndio msingi mkubwa wa chama kwa upande wa kanda ya Serengeti pamoja na kanda ya Viktoria.

Mbele ya waandishi wa habari wabunge hao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kudhaminiwa na Chadema, wametaja sababu kadha wa kadha zinazowafanya kuamua kuachana na Chama hicho.

Sababu za kuondoka chadema.

 • Kutokuheshimu katiba ya chama. Msingi mkuu wa kuanzishwa kwa mageuzi ya mfumo wa vyama vingi ni pamoja na kudai katiba mpya ya Tanzania hivyo ndani ya chadema kumekuwa na kupuuzwa.
 • Demokrasia kutotekelezwa kwa vitendo ndani ya chama kwa mfano;-kukiukwa kwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa;mfano wabunge wenzao wanne ambao ni Mhe.Wilfred Lwakatare, Mhe Joseph Selasini, Mhe.Antony Komu na Mhe David Silinde kufukuzwa uanachama bila kusikilizwa.
 • Kukiukwa kwa haki ya kuhoji matumizi ya michango na fedha za ruzuku mfano wabunge wa viti maalum kila mmoja kwa mwezi anachangia chama sh.1,550,000 tangu mwezi January 2016 mpaka mwezi April 2019 ambapo ni miezi 40. Hivyo kila mmoja wao amechangia chama takribani sh.62,000,000 million ambapo wabunge wa viti maalumu wapo 37 hivyo kuchangia zaidi ya billion 2. Huku fedha hizo kutowekwa wazi matumizi yake na kutoruhusiwa kuhoji.
 • Madaraka kuhodhiwa na wachache wengi wao wakiwa ni wanaume na hivyo kuwepo mwanya wa unyanyasaji wa kijinsia na wakingono.
 • Ndani ya chadema kuna mgawanyiko mkubwa unaotokana na baadhi ya watu kujiona wao ni bora kuliko wengine kwa bahati mbaya sana jitihada zote za kutaka kuondokana na hali hii ili wabaki wakiwa wamoja wanapoelekea uchaguzi mkuu zimeshindikana.
 • Ndani ya chadema kuna makundi ya kibaguzi hadi bungeni kwa wabunge hao uchangiaji katika vikao vya bunge unaenda kwa kufahamiana na wengine kufanywa wapiga makofi na wanaoitwa wabunge maarufu.

 

Sababu za kujiunga na Nccr Mageuzi

 • Itikadi yake ya UTU ambayo msingi wake mkuu ni haki za binadamu.
 • Katiba yake pamoja na mengi mazuri yaliyopo imeweka wazi usawa wa kijinsia mfano makamu mwenyekiti wa taifa na katibu mkuu wake ni mwanamke na kuwa chama cha mfano hapa nchini kwa usawa wa jinsia.
 • Katiba na kanuni za uendeshaji chama zimeziba mianya ya uvunjifu wa amani ndani ya chama na nje ya chama na hivyo kulinda amani ya nchi.
 • Utulivu wa kisiasa ndani ya chama.
 • Chama kinaweka maslahi ya taifa mbele kwanza kabla ya maslahi ya chama na mengine yoyote kwa mfano chama kimejikita kwenye kuboresha elimu ya watanzania kwa hoja na vitendo.Mabadiliko mengi yanafanywa kwenye sekta ya elimu na serikali ya awamu ya tano inatekeleza sera za NCCR Mageuzi

Ni dhahiri kwa wale walioko chadema na wanaondoka hahawezi kushangaa hoja hizo za wabunge.

Hivyo basi kama tunataka kutengeneza taifa la watu wanaojiheshimu na viongozi waadalifu kuna haja mambo kama haya yasemwe ili kuliokoa taifa.