Dunia imekumbwa na kirusi kinachosababisha ugonjwa unaoitwa COVID-19 (Corona) na tayari mataifa kadhaa ulimwenguni yametajwa kukumbwa na janga hili.

Nchini Tanzania visa zaidi ya 6 sasa vya ugonjwa huo wa Corona vimeshatangazwa na mamlaka husika huku tahadhari ikizidi kutolewa na taasisi na watu mbalimbali nchini ili  kuepuka maambukizi ya ugonjwa huo.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa ambaye pia ni mtalaamu wa masuala ya majanga Ndg. James Mbatia amewataka wataanzania kuchukua tahadahari juu ya gonjwa hilo ikiwemo na

  • Kutambua hali iliyoko kwa  usahihi.
  • Kutekeleza maagizo yanayotolewa na mamlaka husika.
  • Kuwa na utulivu wa ndani kwakuwa kirusi hicho ni kipya. Wataalam wanaendelea kutafiti mchana na usiku jinsi ya kupambana nacho hasa katika kupata dawa na chanjo dhidi yake.Kazi hii inafanywa na wataalam hasa wa sekta ya afya sehemu mbalimbali Duniani.Hivyo, taarifa ni nyingi na wakati mwingine zinaweza kuleta mkanganyiko.

Mwenyekiti Nccr-Mageuzi Ndg. James Mbatia akiwa pamoja na Mkuu wa Idara ya uenezi na Mahusiano ya Umma Ndg. Edward Julius Simbeye kwenye mkutano na waandishi wa habari wakizungumza kuhusiana na tahadhari juu ya Corona.

“Nashauri Mamlaka husika ziwe zinatoa taarifa za mara kwa mara ili wananchi wawe na uwelewa wa pamoja jinsi ya kujikinga na kutoa taarifa sahihi za kuwepo kwa wagonjwa mahali popote.Kinga ndio TIBA pekee kwa sasa wakati tukisubiri dawa na chanjo.”-James Mbatia

Wakati huo huo Ndg.Mbatia amewataka watanzania kujijengea tabia na mazoea mapya ya kupokea taarifa na kuzifanyia kazi kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.

Mwenyekiti Taifa Ndg.James Mbatia akizungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya tahadhari dhidi ya janga la corona.

Hata hivyo katika kupambana na janga hili Ndg. Mbatia amewataka watanzania kuwa na utulivu wa ndani kwa kulinda kinga ya miili kwa kuelimishana, kushirikiana na kusaidiana.  “jirani yangu kama hayuko salama, nami pia siko salama”.