Dar es Salaam,

Mwenyekiti wa kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ndg. James Mbatia ameongoza mkutano wa ndani wa majadiliano wa vyama vya siasa ngazi ya Taifa wenye lengo la kutatua migogoro ndani ya vyama ili kujenga uamininifu miongoni mwao.

Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Protea Courtyard jijini Dar es salaam, moja ya ajenda kuu ilikuwa ni kujenga siasa ya maridhiano ya pamoja ili kuweza kuondoa migogoro ndani ya vyama vya siasa pamoja na kujenga jamii yenye umoja.

Viongozi na wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa zaidi ya 30 pamoja na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini, wameudhuria majadaliano hayo, akiwemo Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndg. James Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa kituo cha Demokrasia nchini (TCD), Katibu idara ya oganaizesheni na utawala Taifa-NCCR-Mageuzi ndg. Florian Rutayuga Mbeo, Mkurugenzi Haki za binadam (CUF) ndg. Salvatory Magafu, Naibu katibu mkuu ACT-Wazalendo, Ndg. Hamad Yussuf, wakili wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA Bi. Ester Safi, Balozi Mstaafu ndg. Mohamed Omary pamoja na wawakilishi wengine wa vyama vya siasa na taasisi nchini.

Katibu idara ya oganaizesheni na utawala Taifa-NCCR-Mageuzi ndg. Florian Rutayuga Mbeo pamoja na wawikilishi wengine kwenye mkutano wa majadiliano wa vyama vya siasa nchini

Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu mapema mwaka huu. Huku viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini wito wao mkubwa umekuwa ni kupunguza manung’uniko yanayojitokeza kwenye chaguzi mbalimbali. Lakini pia kuunda tume huru ya uchaguzi itakayosimamia mchakato mzima wa uchaguzi mkuu 2020.

Balozi Mstaafu ndg. Mohamed Omary, moja ya wajumbe kwenye mkutano wa majadiliano wa vyama vya siasa nchini chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania, TCD