Ndugu waandishi wa habari, kama mnavyofahamu nimekuwa nikikitumikia chama cha ACT Wazalendo kwa takribani miaka 5 sasa, nimekuwa nikihudumu kamati mbali mbali za chama mpaka ilipofikia mwezi machi baada ya uchaguzi wa Ngome ambao niligombea kama Mwenyekiti ila sikushinda kutokana na sababu mbali mbali ambazo sitaweza kuzieleza hapa.
Naomba nichukue nafasi hii pia kuishukuru ACT Wazalendo kwa hapa iliponifikisha ila sina budi kusema inatosha kuwa mwanachama wake.

Ndugu waandishi wa habari, naomba kuujulisha umma wa Watanzania kuwa kuanzia siku ya leo tarehe 05 mwezi Julai 2020 ninajivua uanachama rasmi wa chama cha ACT Wazalendo na kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi.

KWANINI NCCR MAGEUZI?

1. Ubora wa muundo wa katiba ya chama jinsia mabavyo imekuwa ikijieleza wazi kusimamia utu, uwajibikai na usawa. Ambao huu umekuwa msingi mkubwa sana kwangu kwa maana ndio wenye kuthamini watu na hali zao.
2. Utayari wa wanachama kunipokea nami nitoe mchango wa ujenzi wa chama hiki. Kama tutakumbuka chama cha NCCR Mageuzi ndio chama cha upinzani kibwa kwenye historia ya kigoma. Ninajiunga nao kwenda kuongeza chachu ya mageuzi ndani ya mkoa wangu wa Kigoma na ndani ya Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Aliyewahi kuwa Afisa wa Chama cha ACT-Wazalendo na baadae kuwa Katibu wa Sera na Tafiti ACT-Wazalendo Vijana Taifa ndugu Luth Kitentya akikabidhiwa kadi ya uanachama na Kamishna wa Mkoa wa Kigoma kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ndugu Frank Ruhasha

YAPI NINAYOTEGEMEA KUYAFANYA JIMBONI?

Naomba nichukue nafasi hii pia kuwafahamisha wanachama wenzangu na wananchi wa jimbo la kigoma kaskazini, kuwa ninatangaza nia yangu ya kugombea Ubunge kupitia NCCR-Mageuzi.
Jimbo la Kigoma Kaskazini ni jimbo ambalo linachangamoto nyingi sana ambazo zinafifiza ukuaji wa kiuchumi kwa wanachi.

Ndugu waandishi wa habari kama ambavyo mnashuhudia kumekuwa na Kuporomoka kwa bei ya Mafuta ya mawese, ukosefu wa miundombinu ya barazara zinazoonganisha kata mbali mbali ambazo zinapitika katika vipindi vyote, migogoro baina ya Gombe na Kata jirani, ukosefu wa soko kwa mazao ya kilimo, Migogoro baiana ya Wanachi na mamlaka za Uvuvi, Ukosefu wa Vituo vya Afya vya kutosha na Uwepo wa shule zenye Kukidhi mahitaji ya msingi ya kufundisha na kujifunza. Hizi ni baadhi ya changamoto ambazo zimenisukuta kutia nia na kuomba chama change cha sasa NCCR Mageuzi kuomba kupeperusha na kuhakikisha tuankwenda kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenda kutatua na kuzimaliza changamoto zinazoikabili jimbo letu na halmashauri yetu kwa ujumla.

Kitentya Luth

NI LAZIMA TUSONGE MBELE. NILAZIMA TUENDELEE KWENDA MBELE.
KAMA HUWEZI KUPAA, KIMBIA. KAMA HUWEZI KIMBIA, TEMBEA.
KAMA HUWEZI KUTEMBEA, TAMBAA, ILA KWA NAMNA YOYOTE ILE LAZIMA TUENDELEE KUSONGA MBELE.