Chama cha NCCR Mageuzi kimepuliza kipyenga cha Uchaguzi  Mkuu wa mwaka huu kwa kufungua dirisha la kuchukua na kurudisha fomu kwa wanaowania nafasi za Udiwani, Uwawakilishi, Ubunge pamoja na Urais kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bi. Elizabeth Mhagama amesema dirisha hili limeanza rasmi tarehe 15 Juni hadi tarehe 08 Julai, 2020.

Bi. Elizabeth amefungua dirisha hilo huku akiwataka wagombea urais wa Tanzania bara pamoja na Tanzania Zanzibar kuwa na wadhamini wasiopungua 200 ndani ya Mikoa kumi (10).

Mwanzoni mwa mwaka huu chama cha NCCR Mageuzi kupitia kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika tarehe 19 Februari, 2020 chama kiliadhimia kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu kwa kusimamisha wagombea katika ngazi zote yaani Udiwani, Uwakilishi katika baraza la Mapinduzi Zanzibar, Ubunge katika bunge la Jamuhuriya Muungano wa Tanzania, Urais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine Bi. Elizabeth ameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea kutoa ushirikiano kwa watanzania katika kufanya zoezi hilo la Uchaguzi liweze kuwa la Amani, Huru na Haki kama Rais alivyokwisha kutamka.

“Tunaamini kabisa Tume itatenda haki katika kutangaza mshindi, kutoa elimu ya mpiga kura kwa Watanzania wote na kwa wakati pamoja na kutekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kusambaza vifaa vya uchaguzi vya kutosha na kwa wakati”-Alisema Bi. Elizabeth

Aidha Bi. Elizabeth amewaomba wapiga kura kutumia haki yao kikatiba kushiriki kikamilifu hasa katika kupiga kura na kujiepusha na matendo yote ya uvunjifu wa amani.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Bi. Elizabeth amefafanua sifa za wagombea Udiwani, Ubunge na Urais wanapaswa kuwa wanaoamini na kujali UTU wetu hakimsingi za kila mtanzania zinapatikana.

Mwenye maadili ya Kitanzania

  • Mwenye Kusimamia maslahi ya wengi dhidi ya wachache, ndani na nje ya nchi.
  • Mwenye kusimami na kutetea katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye uwezo wa kuzuia upitishaji wa sheriambovu, kushirikisha wananchi katika mipango ya maendeleo ya umma na kufanya maamuzi magumu kwamaslahi ya wengi.

Hata hivyo zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea utafanyika katika maeneo ambapo mgombea anapatikana kupitia ofisi ya kata kwa nafasi ya udiwani, Ofisi ya katibu wa Jimbo husika kwa nafasi ya Ubunge na Ofisi ya Katibu Mkuu Makao Makuu ya Chama kwa nafasi ya Urais upande wa Tanzania bara na kwenye Ofisi ya Kamati Maalum ya Halmashauri kuu Zanzibar kwa nafasi ya mgombea wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ikumbukwe kuwa nchi yetu inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge, Wawakilishi pamoja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifikapo Oktoba Mwaka huu.

VIWANGO/GHARAMA YA UCHUKUAJI WA FOMU KATIKA NGAZI MBALIMBALI