Katika kuendelea kusimamia na kutekeleza Itikadi ya UTU, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo Ndg. James Francis Mbatia ametembelea Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga  kukagua Uhai wa chama na kutatua mapungufu yanayokwamisha chama kusonga mbele.

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jimbo hilo Ndg. James Mbatia amesema anaridhishwa na utendaji kazi wa jimbo hilo mpaka sasa ambapo kwa kipindi cha miezi miwili  chama cha NCCR- Mageuzi kimefanikiwa kupata zaidi ya wanachama wapya 13,236 ndani ya jimbo hilo.

Mbatia amesema ameridhishwa kuona wakazi wa jimbo la solwa wakiishi Itikadi ya UTU na misingi yake ambayo misingi yake ni Udugu, Maadili, Usawa, Haki, Imani,Mabadiliko, Uhuru,Wajibu, Asili,Kazi na Maendeleo.

Licha ya kuishi kwenye misingi ya itikadi ya UTU, wananchi wa jimbo hilo wameonekana kutikia kwa kasi sana wito wa mabadiliko chanya hali inayoenda sambamba na kukiunga mkono chama chetu cha NCCR Mageuzi kwa kasi mno. Hali hii imemfanya  Ndugu James Mbatia (M/kiti wa NCCR-Taifa) kuahidi kutatua changamoto zinazowakabili kwa haraka ikiwemo tatizo la usafiri kulingana na jiografia ya eneo hilo kuwa pana ili kuendana na kasi ya vugu vugu la mabadiliko ndani ya jimbo hilo la Solwa.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa Ndg, James Mbatia akipokea ripoti kutoka kwa Viongozi wa Jimbo la SOLWA

Jimbo la Solwa lina wapiga kura zaidi  ya 151,000, kata 26, Matawi 126 na Vitongoji 856  ambapo ziara ya Mwenyekiti wa Chama Taifa Ndugu James Mbatia Katika Jimbo hilo, imeamsha hari mpya ya vugu vugu la mabadiliko.

Licha ya ziara ndani ya jimbo la Solwa Mwenyekiti Ndugu James Mabatia alitembelea pia kwenye majimbo ya Kahama, Msalala pamoja na Ushetu yote kwenye mkoa wa Shinyanga ambapo zaidi ya wanachama 30,000 kutoka vyama vingine vya upinzani walijiunga na chama chetu kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya ziara hiyo.

Zoezi la Upandishwaji wa bendera ya NCCR-Mageuzi, SOLWA