Na Sam Ruhuza

Miaka ya 1995-2000 NCCR- Mageuzi ilikuwa chama Kikuu cha upinzani nchini kwa wingi wa kura za Rais na Wabunge, japo haikufanikiwa kuunda kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) kwa sababu CUF ilikuwa na idadi zaidi ya viti Bungeni kutokea Zanzibar maana haikufanikiwa kupata kiti cha Ubunge Tanganyika, hivyo iliungana na vyama vya UDP na Chadema vilivyokuwa na Wabunge watatu watatu kila chama kuunda kambi ya Upinzani Bungeni!

Japo NCCR- Mageuzi haikuwa KUB, lakini ilikuwa na Wabunge mahili sana waliotoa hoja za kuifanya Serikali kuwajibika ipasavyo!

Mwaka 2000-2010 chama cha CUF kilikuwa Chama Kikuu cha upinzani kwa kushika uongozi Bungeni. Wakati huu walishirikisha vyama vingine vya upinzani kuunda KUB.

Mwaka 2010-2020 Chadema imekuwa ni chama Kikuu cha upinzani Bungeni na Majimboni!

Tumeona NCCR- Mageuzi ilikuwa chama Kikuu cha upinzani miaka 5, kikapoteza muelekeo ná nafasi yake kuchukuliwa na CUF ambayo ilikaa na ukubwa kwa miaka 10, iliposhindwa kuingia Ikulu tumeshudia Chadema ikichukua nafasi hiyo.

Katika kipindi cha CUF kuchukua toka NCCR- Mageuzi na Chadema kuchukua toka CUF hatukusikia shutuma zozote toka NCCR- Mageuzi kuishutumu CUF, wala CUF kuishutumu Chadema, zaidi ya kutulia akili zao kujipanga upya na kutumia makosa yao kama changamoto kujijenga vyema! Hiyo ndio maturity kwenye siasa.

Tupo Mwaka 2020 na Inawezekana kabisa mwezi Oktoba kukafanyika uchaguzi Mkuu. NCCR- Mageuzi Inawezekana kuvuna Wanachama wengi na kujiimalisha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Lengo Kuu la Chama chochote cha siasa ni kuongoza Dola. Washabiki wa mpira watanielewa kuwa Timu yoyote lengo lake ni kuwa Bingwa sawa na Mwana Michezo yeyote lengo lake ni ushindi!

Chama ambacho hakina Mbunge kinapambana angalau kipate Mbunge mmoja! Hayo ni mafanikio makubwa kwao.

Chama chenye Wabunge wachache kinapambana kuongeza Wabunge wengi ili angalau kuunda kambi ya Upinzani Bungeni! Hayo ni mafanikio makubwa sana kwao.

Chama Kikuu cha upinzani kinapambana kichukue Dola! Maana ndio hatua pekee iliyobaki kwao. Ni sawa na timu ya mpira kila mara inaishia nafasi ya pili, inatafuta mbinu za ziada angalau ichukue ubingwa!

Chama Tawala kinakuwa makini kupambana kisitoke Madarakani kirahisi!

Nimeshtuka sana kusoma mitandaoni wafuasi wa chama Kikuu cha upinzani wakitoa shutuma nyingi sana na maneno ya kejeli kwa Viongozi na chama cha NCCR- Mageuzi kupokea Wanachama toka vyama vingine vya Upinzani. Nimejiuliza kama wafuasi/washabiki/Wanachama wanajitambua?!?

Nimeandika mtiririko wa Vyama vya Upinzani na ukuu wake. Mbona hatukusikia shutuma hizo wakati NCCR- Mageuzi na CUF zinaondoka kwenye ukuu wao??!  Kwanini leo hao wengine wachukie kuona wenzao wanafanya vyema?! Kwanini hata wasifurahi kuona Wanachama wao bado wapo upinzani??! Au kwao Mwanachama wao kuhamia ccm ni bora zaidi kuliko kuhamia chama kingine cha upinzani??!!

Nimejiuliza lengo la Chama Kikuu cha upinzani ni nini??!

Inaelekea wafuasi wa hicho chama wanataka kusalia kuwa Wapinzani Bungeni na hakuna malengo ya kwenda Ikulu!

Ni utaratibu wa wapiga kura kukushusha kutoka kuwa chama Kikuu cha upinzani ili ujitafakari zaidi ulipokosea maana muda huu ni wa Chama Kikuu cha upinzani kuwaza kwenda Ikulu!

Nasoma mtandaoni eti NCCR- Mageuzi wameingia Dili ya kupewa viti ili kiwe chama Kikuu cha upinzani Bungeni!

Hii Habari hata kama ni ya kweli, wewe chama Kikuu cha upinzani inakukera nini wakati wewe utakuwa ndio chama tawala??!

Ninashindwa kuelewa nini hasa lengo lao, Je mnataka muendelee kuwa chama cha upinzani hadi lini?!

Je, mmekosa mbinu za kuingia Ikulu?!

Badala ya kuwaza kuingia Ikulu, mnaishia kuitukana na kuikejeli NCCR- Mageuzi eti wanataka kuchukua nafasi yenu Bungeni ya kuwa Chama Kikuu cha upinzani, hivi mnakosea wapi??!

Huwa sipendi kabisa na andiko hili ni mara yangu ya kwanza kuongelea maelewano ya vyama vya Upinzani, maana ni Aibu kubwa kuongelea hayo. Wakati Wananchi wamechoshwa na Serikali iliyopo wanahitaji kupata Serikali mbadala, wanashudia shutuma ambazo ukizifuatilia ni wivu tu wa nafasi ya chama katika uongozi wa Jamii!

Ninawashauri hiki Chama Kikuu cha upinzani kujipanga upya kupambana na ccm. Hii nafasi ya Upinzani hamuwezi kukaa nayo milele, ni lazima mbadilike waingie wengine na ninyi msonge mbele, ila kama nimepoteza Dira, basi ndio Byebye tena!!

NCCR- Mageuzi kwakuwa ilikwisha chama Kikuu cha upinzani nchini kina ukomavu wa uongozi na kinaendelea kujijenga na kujiimalisha zaidi hivyo kwa kupitia uzoefu wake kipo tayari kabisa kuingia Ikulu na kuacha ushindani wa chama Kikuu cha upinzani kwa ccm na hao wanaotamani kuendelea kuwa wapinzani!

Kwa muitikio wa Wananchi kuielewa NCCR- Mageuzi ni matumaini yangu hadi kipindi cha uchaguzi Mkuu kura nyingi zitaangukia kwa NCCR- Mageuzi na hivyo kuongoza Dola.

Tanzania ni yetu sote