Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa kumekuwepo na taarifa nyingi za sintofahamu kuhusu ustawi wa chama chetu. Hasa wanachama wapya wanaojiunga na chama chetu.

Ikumbukwe kuwa chama chetu cha NCCR-Mageuzi ndiye muasisi wa mageuzi nchini, kuanzia kamati ya Taifa ya mabadiliko ya katiba yaani “National Committeefor Constitutional Reform {NCCR} iliyoundwa tarehe 12, June 1991.

Katika Uchaguzi mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi vya siasa wa mwaka 1995, tulifanikiwa kupata wabunge 19 lakini kutokana na udhaifu wa kuendesha taasisi na migogoro ya ndani ya chama, Uchaguzi uliofuata wa mwaka 2000 tulipoteza wabunge wote 19.

Wakati hayo yakitokea Kwa kipindi cha miaka 20 tumejifunza mengi tukiongozwa na Itikadi yetu ya UTU ambayo ni kati ya ITIKADI zilizo bora Duniani.

Hivi sasa ndani ya chama chetu kuna Uongozi unaofuata misingi ya Utikadi yetu ya UTU ambayo ni Udugu, Maadili, Usawa, Haki,Imani ,Mabadiliko , Uhuru, Wajibu, Asili, Kazi na endelezo.

Makamu Mwenyekiti NCCR-Mageuzi Tanzania Bara Bi. Angelina John Mutahiwa  akimkabidhi kadi ya Uanachama ya NCCR-Mageuzi aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti na Mshauri wa ACT Wazalendo Ndg. Yeremia Kulwa Maganja

Hivyo basi tunawaomba watanzania wapuuze taarifa za uzushi, uzandiki na za kichochezi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti ukiwa unaitwa “WARAKA NAMBA MOJA WA MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA WA MWAKA 2020 KWA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.

Waraka huo ulitolewa tarehe 08.03.2020 Kwa nia ovu ya kuchafua Utu wa chama chetu. Katibu Mkuu ndugu Elizabeth Muhagama  alitoa  malalamiko yetu rasmi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania {TCRA} tarehe 12.03.2020 na kumpatia nakala msajili wa vyama vya siasa kukanusha waraka huo na kuiomba TCRA kufanya Uchunguzi wake kwa kina na kuchukua  hatua  stahiki  za kisheria wakati huo huo Mwenyekiti wetu wa Taifa Ndugu James Mbatia alikanusha waraka huo tarehe 10.03.2020 alipokuwa anazungumza na wahariri wa Mwananchi Communication Limited.

Aidha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 20{1}inasema “Kilamtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine,na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na kuanzisha na kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.”

Hata hivyo baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa tarehe 27.07.2019 ulitoa maagizo kwa halmashauri kuu ya Taifa kuandaa mpango kazi wa mwaka 2020 na mpango kazi huo ulipitishwa  tarehe 19.02.2020  hivyo  basi chama chetu kimeendelea kufanya kazi za kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini kwa mafanikio makubwa tukianzia mkoa wa mbeya tulipata wanachama wapya 9540, Mkoa wa shinyanga wanachama wapya 20,645, Mkoa wa kigoma wanachama wapya 29,495 na kufikisha Jumla ya wanachama 59,680 kwa kipindi cha muda mfupi.