Habari Maalumu Articles

 Kwaheri ACT-Wazalendo, hodi NCCR-Mageuzi

Ndugu waandishi wa habari, kama mnavyofahamu nimekuwa nikikitumikia chama cha ACT Wazalendo kwa takribani miaka 5 sasa, nimekuwa nikihudumu kamati mbali mbali za chama mpaka ilipofikia mwezi machi baada ya uchaguzi wa Ngome ambao niligombea kama Mwenyekiti ila sikushinda kutokana na sababu mbali mbali ambazo sitaweza kuzieleza hapa.
Naomba nichukue nafasi hii pia kuishukuru ACT Wazalendo kwa hapa iliponifikisha ila sina budi kusema inatosha kuwa mwanachama wake.

BREAKING NEWS: NCCR-Mageuzi yavuna tena wanachama zaidi ya 250, Mara.

BREAKING NEWS: NCCR-Mageuzi yavuna tena wanachama zaidi ya 250, Mara.

Ziara inayoendelea katika mikoa ya kanda ya ziwa inayoongozwa na Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma ndugu Edward Julius Simbeye inaonyesha kuwa na matokea chanya siku baaada ya siku. Zaidi ya wanachama 250 kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini wakiwemo viongozi  mbalimbali wa majimbo na kata kutoka  mkoani mara hii leo wametangaza rasmi kujiunga na NCCR-Mageuzi na kukabidhiwa rasmi kadi za uanachama na ndugu Edward Simbeye.

read more
Simbeye aongoza ziara ya kukagua uhai wa chama kanda ya ziwa.

Simbeye aongoza ziara ya kukagua uhai wa chama kanda ya ziwa.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha watia nia wa Ubunge ndani ya NCCR-Mageuzi kuelekea uchaguzi mkuu 2020, shughuli za ujenzi wa chama pamoja na kukagua uhai wa chama zinaendelea nchi nzima. 

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma Ndugu Edward Julius Simbeye ameongoza shughuli hizo kwa mikoa iliyopo kanda ya ziwa.

read more
 NCCR-Maguzi yawanoa watia nia wake wa Ubunge 2020

 NCCR-Maguzi yawanoa watia nia wake wa Ubunge 2020

“Viongozi uandaliwa, viongozi hawaokotwi kwenye majalala” hii ni kauli ambayo imekuwa ikisisikika mara kwa mara kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, ndugu James Francis Mbatia (Mb). Dhana kuu ya kauli hii inaakisi mienendo na tabia za viongozi wengi tulio nao sasa ambao mara nyingi wamekuwa wakionesha hali ya sintofahamu katika nafasi zao za majukumu.

read more
Vuguvugu la Mageuzi Arusha

Vuguvugu la Mageuzi Arusha

Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo Ndugu JAMES FRANCIS MBATIA amezitaka mamlaka zinazosimamia uchaguzi kuwatendea haki Watanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba ili kupata viongozi wanaostahili kwa maslahi mapana ya mama Tanzania.

read more
Mwelekeo wetu NCCR-Mageuzi

Mwelekeo wetu NCCR-Mageuzi

Karibu Watanzania NCCR-Mageuzi chama kinachojali UTU wa binadamu na viumbe hai wote hapa Duniani. Chama kinachoamini katika Diplomasia ya Maridhiano Amani na Utulivu wa Nchi yetu. Chama chetu kinalenga kuwa na Vijana wafuasi wa Amani na Umoja wetu kama Taifa, siasa za masuala baadala ya zile za kujadili watu na kujadili matukio.

read more

Pin It on Pinterest