Ziara inayoendelea katika mikoa ya kanda ya ziwa inayoongozwa na Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma ndugu Edward Julius Simbeye inaonyesha kuwa na matokea chanya siku baaada ya siku. Zaidi ya wanachama 250 kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini wakiwemo viongozi  mbalimbali wa majimbo na kata kutoka  mkoani mara hii leo wametangaza rasmi kujiunga na NCCR-Mageuzi na kukabidhiwa rasmi kadi za uanachama na ndugu Edward Simbeye.

Viongozi na wanachama hao ambao wamtengaza kujiunga na NCCR-Mageuzi hii leo Julai 03, 2020 wametoka kwenye majimbo mawili ya mkoani Mara, Jimbo la Tarime Mjini pamoja na Jimbo la Rorya.

Mapema hii leo katika Jimbo la Tarime Mjini, Ndugu Edward Simbeye aliwapokea wanachama zaidi ya 5o kabla ya kuwapokea viongozi na wanachama zaidi ya 200 kutoka jimbo la Rorya wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa Vijana wa CHADEMA Wilaya ya Rorya Ndugu Steven Aroma Ryaga na hivyo kufanya kuwa idadi ya wanachama 250.

Viongozi wengine waliojiunga na NCCR-Mageuzi kutoka jimbo la Rorya ni pamoja na kiongozi wa kata wa Kirogo, Roche ,Raranya, Mkoma , Nyahongo,Bukura pamoja na kata ya Tai.