Mapinduzi ya kisiasa nchini yanaonekana kuzidi kushika kasi. Wanasiasa sasa ni wazi ndo wameshika nguzo ya nyumba kubwa, Mama Tanzania. Kwa sasa si ajabu tena kuona kiongozi akihama kutoka chama kimoja cha siasa kwenda kingine, na hii ni kutokana na utashi pamoja na matakwa ya kikatiba ambapo mtu yeyote ana uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa atakapoona inampendeza.

Hivi karibu kumekuwa na majina makubwa yakitajwa hasa baada ya kuvihama vyama vyao.  Anthony Calist Komu ni mwanasiasa mkongwe nchini. Mchango wake kwenye siasa ya Tanzania umeanza kuonekana katika kipindi cha miaka ya 90 ambapo anatajwa kuwa ni miongoni mwa wanamageuzi waliopigania mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Komu kwa sasa ni Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha wananchi wa jimbo la Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hivi karibuni ametajwa sana hasa kutokana na nia yake thabiti ya kutangaza kuamua kuachana na chama chake sasa cha CHADEMA mara tu baada ya kumaliza muhula wake wa Ubunge kwenye jimbo la Moshi Vijijini kupitia CHADEMA mwaka huu. Mwenyewe ameweka bayana kuwa si siri tena, anarejea kwenye chama chake cha zamani cha NCCR-Mageuzi, chama ambacho alikipigania katika harakati za kudai mabadiliko/Mageuzi ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.

ANTHONY KOMU NI NANI?

Anthony Calist Komu ni mchumi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na ni Mbunge wa moshi Vijijini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Mnamo Mwaka 1988 Komu alikuwa ni mmoja wa viongozi wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam aliyeongoza harakati za kuiondosha CCM katika kuhodhi vyama vya wanafunzi kupitia Uvccm nakuwezesha kuanzishwa vyama huru vya wanafunzi Daruso.

Katika harakati hizo ndipo alipata bahati ya kufahamiana na watu waliokuwa na kiu ya uwepo wa vyama vingi na kuunganisha nguvu na kufanikiwa kuanzishwa kwa Multi Party Streering Committee ikiwa na watu 11. Kamati hiyo ndiyo iliyokuja kuzaa baadaye kamati ya marekebisho ya katiba “The National Committee for Constitutional Reforms (NCCR)iliyokuwa Tanzania Bara na “Kamahuru” kwa upande wa Zanzibar.

Tukio hilo lilitokea  katika mkutano wa wananchi ulifanyika kwa siku mbili tarehe 11 na 12 june 1991 jijini Dares salaam.

Moja ya maazimio katika mkutano huo lilikuwa kuitaka serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wakati huo ndani ya mwaka mmoja kurekebisha sheria na kuhalalisha mfumo wa vyama vingi nchini, vinginevyo wananchi wangeanzisha vyama vyao vya siasa.

Hili likawezekana na kufanikisha kuanzishwa kwa NCCR-Mageuzi National Convention for Contruction and  Reforms-Mageuzi: akiwa mwanachama wa kadi Na.7 na kufanikiwa kukitumikia chama cha NCCR-Mageuzi katika nafasi mbalimbali ngazi ya taifa Ikiwemo ya Mkurugenzi Mtendaji mpaka mwaka 2003 alipojiunga na Chadema.

Komu ni mwanasiasa mpole, asiyejikweza, mtoaji ndani ya chama, akiwa chama cha NCCR-Mageuzi Komu alikuwa mtu wa Oganaizesheni kampeni na Utawala mnamo Mwaka 2000,Mwaka 2002 alikuwa katibu wa mkoa wa Dar es salaam.

Antony Calist Komu alijiondoa mwenyewe kwa ridhaa yake kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na kuelekea chama cha CHADEMA mwaka 2003 kutokana na migogoro iliyokuweko ndani ya chama kwa wakati huo.

Hivi karibuni Anthony Calist Komu ameomba ridhaa ya kujiunga na chama chetu (NCCR-Mageuzi) tunatarajia kuwa na Anthony Calist Komu Muadilifu na mtu mwenye nidhamu na chama alichokiasisi.

Komu akiwa chadema amewahi kuwa mkurugenzi wa fedha wa chama hicho. Ndani ya chadema amekuwa afisa fedha kwa muda mfupi sana na baadaye kuwa mkurugenzi wa fedha na Utawala, nafasi aliyoitumikia kwa miaka 14 mfululizo.

Kwa kupitia nafasi hiyo aliweza kuwa katibu wa baraza la wadhamini wa vikao vyote vya kitaifa na kufanya kazi hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa.

Aliondoka katika nafasi hiyo mwaka 2016,kwa moyo mkunjufu mara baada ya marekebisho ya taratibu za uendeshaji zilizowaondoa wabunge katika nafasi za utendaji,

Akiwa Chadema Chama kilipata mafanikio makubwa ikiwemo ya ukuaji wa ruzuku kutoka sh. Million 5 kwa mwezi mwaka 2000 hadi zaidi ya sh. Milioni 300 mwaka 2015. Aliweza kuanzisha miongozo mizuri ya usimamizi wa fedha na rasilimali, kubuni mbinu mbalimbali za kupata rasilimali na kuzitumia vyema kwa maendeleo ya chama na kusimamia kikamilifu, kutengeneza kanuni sahihi iliyotasfili michango ya kikatiba ya wabunge wa chadema na yeye akiwa ni mmoja wa wabunge waliochangia michango hiyo ya kila mwezi kwa mujibu wa maelekezo ya chama,

Lengo la fedha hizo zilikadiliwa kuwa zingefika shilingi 4.2 billion hadi kumalizika kwa bunge hili zingetumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao 2020. kwa bahati mbaya kusikia minong’ono kuwa fedha hizo nazo zilishatumika kwa malengo mengine.

Anthony Calist Komu ameshiriki kuanzisha na kujenga taasisi zinazopigania Demokrasia, Utawala wa sheria na haki za binadamu Tanzania (TCD)

Huyu ndio Anthony Calist Komu, shujaa wa vita aliyevaa barakoa ya magaeuzi nchini, akizipigania taasisi kwa jasho na damu pasipo kuonyesha sura yake. Huyu ni mpiganaji ambaye hakuwahi kuonyeshwa sura yake pindi anapofanya majukumu yake. Amefanya makubwa na tunamtarajia kufanya makubwa ndani ya barakoa yake ya mageuzi. Anthony Calist Komu ni Muasisi wa Mageuzi nchini na sasa ameomba ridhaa ya kurudi kwenye nyumba aliyoiasisi ya NCCR MAGEUZI kutokana na kuridhishwa na Itikadi ya UTU yenye kusimamia Ukweli, Uzalendo, Uadilifu, Usawa, Imani, udugu, Haki, Wajibu pamoja na kazi endelezo